Mwalimu - Christopher Mwakasege
Diamond Jubilee 17 January 2016
SEMINA YA KUPANDA NA KUVUNA.
Bwana Yesu asifiwe , leo tunapo angalia somo hili nataka tuangalie sana IMANI ILETAYO MATOKEO
Msisitizo haupo katika sadaka bali kwenye ni kwenye Imani na msisitizo haupo kwenye kupanda na kuvuna bali upo kwenye Imani. Japo kuna watu huwa wanaambatanisha na maombi wanapotoa sadaka lakini bado msisitizo upo kwenye Imani.
Waebrania 11:31 ‘’ 31Kwa imani, Rahabu, yule kahaba, hakuangamizwa pamoja na wale waliomwasi Mungu, kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi.
Msisitizo hapa upo KWA IMANI. Na sio ukahaba au wale wapelelezi bali msisitizo hapa ni Imani. Na ndio maana biblia inaonesha matokeo ya Imani yake.
Yoshua 2:8-13 8Kabla wale wapelelezi hawajalala, Rahabu akawaendea huko juu darini, 9 akawaambia, “Ninajua kuwa BWANA amewapa nchi hii na hofu kuu imetuangukia kwa sababu yenu, kiasi kwamba wote waishio katika nchi hii wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yenu.
10Tumesikia jinsi BWANA alivyokausha maji ya Bahari ya Shamua kwa ajili yenu mlipotoka Misri, pia lile mlilowatendea Sihoni na Ogu, wafalme wawili wa Waamori mashariki ya Yordani, ambao mliwaangamiza kabisa. 11Tuliposikia juu ya hili, mioyo yetu iliyeyuka na kila mmoja alikosa ujasiri kwa sababu yenu, kwa maana BWANA Mungu wenu ni Mungu aliye juu mbinguni na duniani chini. 12Sasa basi, tafadhali niapieni kwa BWANA, kwamba mtaitendea hisani jamaa ya baba yangu, kwa kuwa mimi nimewatendea hisani. Nipeni ishara ya uaminifu. 13kwamba mtayahifadhi maisha ya baba yangu na mama yangu, ndugu zangu wa kiume na wa kike, pamoja na wale wote walio wa kwao na kwamba mtatuokoa na kifo.’’
Hii habari tunajifunza sana Imani inapohakikishwa mavuno unapotoa sadaka ya mbegu. NA KUMBUKA HILI LITAKUSAIDIA, Imani ya Rahabu haikuwa kwenye sadaka au maombi au matendo ya kukaribisha wapepelezi balli ilikuwa kwenye matokeo ya Imani yake alipotoa ile sadaka.
Fahamu sana umuhimu wa Imani hizi unapotoa sadaka yako.
USIWEKE IMANI YAKO KWENYE SADAKA BALI WEKA IMANI YAKO KWA MUNGU.
Sadaka haisukumi jibu la Mungu Bali Mungu ndiye anayejibu. Na utaona mwingine ameweka Imani yake kwenye maombi na yasipojibiwa anapata shida sana. Ila kumbuka hili weka Imani yako kwa Mungu na yeye atakusaidia kwa kupitia Imani uliyoiweka kwake.
Waebrania 11:1 ‘’ Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana’’
Waebrania 11:6 ‘’ 6Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana ye yote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba Yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.
Warumi 10:17 ‘’Basi Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo.
Yakobo 2: 17,20 ‘’ Vivyo hivyo, imani peke yake kama haikuimbatana na matendo, imekufa, 20Je, wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani bila matendo haifai kitu?
ZINGATIA HAYA. IMANI BILA MATENDO IMEKUFA NA IMANI ISIPOKUWA NA MATENDO HAIZAI.
Sasa Twende tutafsiri ile KWA IMANI RAHABU YULE KAHABA.
Sasa Toa neno Imani, hapo na weka ile ya Waebrania 11;1 itasomeka hivi KWA KUWA NA UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO , , Rahabu, yule kahaba, hakuangamizwa pamoja na wale waliomwasi Mungu, kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi.Weka na Waebrania 11:6 , endeleza itasomeka hivi KWA KUWA ALITAKA KUMPENDEZA MUNGU NA ALIAMINI YA KUWA HUYU MUNGU YUPO NA KWAMBA ANAVYOMTAFUTA ATAONEKANA KWAKE NA KUMPA THAWABU
IMANI INAYOKUHAKIKISHIA MAVUNO UTOAPO SADAKA YA MBEGU/KAMA MBEGU.
Msisitizo wa ujumbe wa leo haupo kwenye sadaka au mavuno au maombi yanayoambatana na sadaka bali upo katika imabi
Ebrania 11:31
Joshua 2:8-13
Mara nyingi tutoapo sadaka tunaweka imani yetu kwenye sadaka.
Au tunaweka Imani kwenye maombi.
Ebrania 11:1
Ebrania 11:6
Rumi 10:17
Yakobo 2:17-20
Imani huja kwa kusikia. Rahabu alikuwa na Imani na Mungu wa Israel(Rahabu hakuwa Myahudi) kwa uaminifu ambao Mungu aliuonesha kwake.
Rahabu alisikia habari za Israel na kuona.
Mbegu kazi yake kubwa ni kubeba future. Unapotoa sadaka ta mbegu weka imani yako kwa MUNGU na kwa uaminifu wake.
Imani ina tabia...unaweza ukawa nayo na isikusaidie.
Hatuwezi kifikia standard ya maisha MUNGU ayatakayo tuyaishi pasipo msaada wake.
MAENEO 5 YATAKAYOKUSAIDIA KUJENGA IMANI YAKO KUKAA MAHALI HUSIKA AU KUPATA IMANI KAMA HAIPO AU KUIRUDISHA IMANI ILIYOPOTEA.
1. kuitambua na kuipokea mbegu.
2 korintho 9:10,11
Mungu anatoa mbegu na anatoa na mkate. Mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kwa ahili ya kula.
Mfano: umepewa 20,000 unajuaje ipi ni mbegu na ipi ni mkate.
Kilichobadilisha nyumba ya Rahabu kutoka kiwa mkate na kuwa mbegu
Galatia 6:7
2 korintho 9:6
2. Kwanini MUNGU amekupa hicho ulichonacho ukitoe kama mbegu
2 korintho 9:10-12
Watu wengi tuna sababu zetu za kutoa sadaka ya mbegu na ni muhimu sana kumuuliza Mungu ni kwanini ametaka utoe mbegu. Sababu moja wapo ni kuongeza kiwango chako cha ukarimu.
Hukubaliki mbele za Bwana kwa usichonacho bali kwa kile ulochonacho.
Muulize Mungu kwanini anataka utoe sadaka kama mbegu na kwa ajili ya nin.
Mbegu ni kwa ajili ya wewe kupata kile kilichopotea
Hekima ya Biblia inasema fikiri kwa ajili ya kesho.
Sababu nyingine ni kukuandaa kwa ajili ya new season.
Mbegu ina season ya kuleta mavuno. Na kupalilia na kunyeshea maji. Maana yake kukazia lile neno likilotumika wakati wa kupanda mbegu.
3.kujua aina ya arthi au udongo wa kupanda hiyo mbegu
Luka 8:11-15
Mbegu ni neno la Mungu. Kama unepewa Hela ili iwe mbegu lazima iambatane na neno la MUNGU na isipoambatana na neno la MUNGU haiwi mbegu ni hela tu. Kupanda mbegu bila maombi utapanda sehemu isiyo sahihi na hutapata mavuno.
Hali ya ardhi/udongo haibadilishwi na hali ya
mbegu yako. Isipokuwa hali ya udongo/ardhi inabadilisha hali ya mbegu yako.
Mungu anapokuelekeza kutoa ana sababu yake.
Mugu peke yake ndio ukimpa mbegu anaweza kuiua na kuikuza tena na ikazaa matunda.
Mungu lazima aiue mbegu ili kuikuza mana mbegu isipokufa haiwezi kuzaa. Mbegu yoyote yenye thamani kwako;
a) unaweza ukaila
b) unaweza usiipande na kuiweka tu ukafurahia kuiona.
Ndio mana lazima MUNGU aiue kwanza mbegu ili kuiotesha tena.
Rahabu alitambua ya kuwa kuna msaada kwa MUNGU wa israel pamoja na kwamba hakuwa mkristo.
Badilisha IMANI yako kama Rahabu alivofanya kwa kubadilisha matumizi ya nyumba yake kutoka kuwa dangulo na kuwa sadaka. Rahabu alichukua risk kubwa ili kulinda IMANI yake juu ya MUNGU wa Israel.
Imani inakutunza na inakutoa na inakupa uvumilivu mpaka kufikia season ya mavuno. Neno linasema utavuna kwa wakati wake usipozimia Roho. Ukiona unachoka lichunguze like neno la IMANI.
Sadaka ni devine invitation ya MUNGU ili kutengeneza katika maisha yako...
Shukrani kwa dada yetu Josephine kwa kutuandalia dondoo hizi ili nawewe msomaji wetu ujifunze
0 maoni:
Chapisha Maoni